Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti iliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 walikufa baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo. Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au huduma za reli, hali inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni. Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu. Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano. Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo. Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."HABARI KWA KISWAHILI
vendredi 30 juillet 2010
WAOKOAJI NCHINI DRC, WAENDELEA NA SHUGHULI ZA UOKOZI
Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti iliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 walikufa baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo. Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au huduma za reli, hali inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni. Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu. Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano. Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo. Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."jeudi 29 juillet 2010
VIONGOZI WA TARAFA WATEULIWA
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewateuwa alhamisi hii Julay 29-2010 viongozi wapya wa tarafa mbalimbali zinazo unda mikoa ua Burundi. Hata hivyo baadhi ya tarafa hazikupata viongozi wapya kwani kumekuwa na utata kuhusu uteuzi wa viongozi wa tarafa kuhusiana na tarafa ambazo madiwani kutoka muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC-IKIBIRI walinyakua ushindi lakini baadae kukana kukaa barazani. Mathalan katika baadhi ya Mikoa ya Bujumubura vijijini jumla ya Tarafa 11, tarafa 4 pekee ndizo zimepata viongozi. Katika Manispaa ya jiji la Bujumbura tarafa 3 pekee jumla ya 13 ndizo zimewapata viongozi wapya ikiwa ni pamoja na Kamenge Buterere na Rohero. Mkoani Bururi tarafa 3 ndizo zimewapata viongozi ikiwa ni pamoja na Matana,Vyanda na Rutovu jumla ya tarafa 9. jumla ya tarafa 129, wameteuliwa viongozi 106.
WYCLIF JEAN APANIA KUGOMBEA URAIS NCHINI HAITI
Familia ya mwanamuziki aliyezaliwa Haiti imesema Wyclef Jean anafikiria kugombea urais nchini humo. Lakini nyota huyo wa kundi la Fugees, ambaye aliteuliwa kama balozi wa nchi hiyo mwaka 2006, hajaamua bado kama agombee nafasi hiyo ya miaka mitano.Haiti ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi mwezi Januari iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000. Taarifa kutoka familia yake ilisema Wyclef "anajali" sana maslahi ya kwao. Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kuwepo uvumi huko Haiti kuwa Wyclef anajiandaa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Wagombea wana nafasi ya kujiandikisha mpaka ifikapo Agosti 7. Ilisema: " Namna Wyclef anavyojali maslahi ya kwao hauna mipaka kabisa na ataendelea kuisaidia nchi yake bila kujali kama yeye ni sehemu ya serikali. "Kwa wakati huu, Wyclef Jean hajatangaza nia yake ya kugombea Urais Haiti. Iwapo, na wakati, uamuzi utakapochukuliwa, vyombo vya habari vitapewa taarifa haraka iwezekanavyo."

Rais aliye madarakani kwa sasa Rene Preval anazuiwa na katiba kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine. Wyclef, anayeishi New York, ni mwanzilishi wa wakfu wa kusaidia binadamu ya Yele Haiti, na amechangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa misaada tangu kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi. Mwanamuziki huyo na mzalishaji wa muziki, anayejulikana zaidi sasa kwa kushirikiana na mwanamuziki nyota wa miondoko ya Pop kutoka Colombia Shakira, anajulikana sana Haiti ambapo nusu ya watu wote nchini humo wana umri wa miaka 21.MKUTANO WA NCHI WANACHAMA WA CEPGL WAANZA MJINI GISENYI
mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za maziwa makuuCEPGL ambazo ni Rwanda, Burundi, na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wanakutana mjini Gisenyi nchi Rwanda tangu alhamis hii Julay 29.2010 kwenye makao makuu ya CEPGL. Mawaziri hao watajadili kuhusu juhudu za kuimarisha shirika la CEPGL. kwenye ajenda ya mkutano watagusia pia kuhusu swala la wanachama kulipia malimbikizo ya michango yo kwenye shirika hilo.
mercredi 28 juillet 2010
CHAMA CHA CNDD FDD CHAIBUKA MSHINDI WA VITI 32 HUKU UPRONA IKIPATA VITI 2

Kulingana na matokeo ya muda yaliotolewa kupitia muungano wa vyombo vya habari nchini Burundi chama tawala cha CNDD FDD cha rais waé sasa Pierre Nkurunziza kimejipatia viti 32 katika baraza la seneti huku chama UPRONA kikipata viti 2. viti hivyo 2 vyama chama UPRONA vilipatika kimoja kutoka Mkoani Bururi huku kingine kutoka jijini Bujumbura ambapo inasemekana kuwa kulikuwa na maelewano baina ya wagombea wa CNDD FDD na UPRONA. juhudu za maelewano hazikufua dafu huko Mkoani Mwaro ambapo wagombea waliochaguliwa ni kutoka chama CNDD FDD. vyama kutoka muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC IKIBIRI havikushiriki uchaguzi tangu pale vilipo lalamikia tume huru inayo anda uchaguzi kuvuta matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa baraza la madiwani, wajumbe ambao ndio wanaowachaguwa wanaseneti kiulingana na katiba ya Burundi. katiba ya Burundi inaamuru kuwashirika watu kutoka kabila la watwa, hivyo watwa 3 wanalazimika kuteuliwa pamoja pia na ma rais wa zamani wa Burundi.
WATU 152 WAMEUAWA KATIKA AJALI YA NDEGE NCHINI PAKISTAN
Ndege hiyo, iliyokuwa katika safari kutoka Karachi kwenda Islamabad inaendeshwa na kampuni Hapakuwa na taarifa za awali kubaini chanzo cha ajali. Ingawa imeelezwa eneo hilo lilikuwa limetandwa na ukungu.Televisheni za Pakistan zilionyesha picha za mabaki ya ndege yakiwaka moto, huku helikopta za uokoaji zikiranda juu.binafsi ya Airblue, ilianguka kwenye vilima vilivyoko kaskazini mwa jiji wakati ikijiandaa kutua.Airblue ndiyo kampuni kubwa zaidi ya ndege binafsi, miongoni mwa mashirika yaliyoibuka nchini Pakistan katika miaka ya karibuni.
Kampuni hiyo na idara ya usimamizi wa safari za ang
a hawadhani ndege hiyo ilikutwa na matatizo ya kiufundi wakati ikiondoka Karachi.Wanasema hapakuwa na dalili za hitilafu ya kiufundi katika mawasiliano kati ya rubani na mnara wa kuongozea ndege wa Karachi.
Hata hivyo, maafisa wa uwanja wa ndege waliieleza BBC kuwa ndege mbili zilizokuwa zitue kwenye mji huo mkuu zilikataliwa kabla ya ajali hiyo ya Airblue, katika ajali kubwa zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Pakistan.
Ingawa sekta ya safari za anga imekuwa kwa kasi, wakosoaji wanasema viwango vimekuwa chini na haviendani na ukuaji wa huduma.
Marubani hulalamika wanalazimishwa kuruka kwa saa za ziada, jambo linalosababisha uchovu, ingawa mashirika ya ndege yanakana madai hayo.mtiaz Elahi, mwenyekiti wa Capital Development Authority, mamlaka inashughulikia dharura, alisema ajali hiyo "inavunja moyo".
"Ni janga kubwa, na ninaweza kuthibitisha kwa uchungu kwamba hapakuwa na watu waliosalimika," alilieleza shir
ika la habari la Associated Press.Ndege hiyo, inayosemekana kuwa ni muundo wa Airbus A321 ikiwa na abiria 146 na wafanyakazi sita ndani yake, inaaminika kuwa iliondoka Karachi saa mbili kasorobo asubuhi majira ya huko.Awali, Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, ilisema watu wasiopungua watano walikuwa wamenusurika kifo na kupelekwa hospitalini, lakini maafisa wa maeneo hayo baadaye walisema taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Televisheni za maeneo hayo zilionyesha vipande vya mabati na chuma vikining'inia kutoka juu ya miti na kutapakaa ardhini.Kifaa cha kutunza kumbukumbu za safari kimekwishapatikana.
Maafisa wanasema waokoaji waliokuwa wakitafuta watu walionusurika, walikuwa wakitumia mikono mitupu kufukua mabaki hayo. Eneo la ajali lililoko kwenye mlima mkali, halifikiki kwa barabara.
mardi 27 juillet 2010
TUME HURU INAYO ANDAA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI CENI YATANGAZA MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI WA WABUNGE
BUJUMBURA LE 27.7.2010: Tume huru inayo andaa uchaguzi nchini Burundi CENI imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya ijumaa iliopita julay 23 mwaka 2010. Matokeo hayo yabaini kuwa chama cha CNDD FDD kimepata viti 81 bungeni huku chama UPRONA kikipata wabunge 17 na chama FRODEBU NYAKURI kikiridhika na wabunge 5. imesalia kuwateuwa wabunge 3 kutoka kabila la watwa wataotoka katika Mikoa ya Cibitoke, Karusi na Mji mkuu Bujumbura. tume hiyo inayo simamia uchaguzi CENI imesema raia walioshiriki uchaguzi wa wabunge imefikia asilimia 66. Ucahguzi wa wanasneta watazamiwa kufanyika siku ya jumanne Julay 28 ambapo kila Mkoa utwakilisha wajumbe 2 kutoka makabila ya wahutu na watutsi. tume huru CENI imetangaza kwamba vyama vya CNDD FDD na UPRONA ndivyo vitavyo wania viti vya uanaseneti. hata hivyo katika baadhi ya Mikoa chama UPRONA kimeshindwa kuorodhesha wajumbe kutoka katika kabila la wahutu. katiba ya Burundi inaagiza kwamba ma rais wa zamani wanaingia barazani moja kwa moja wakimaliza uongozi wao. Domitien Ndayizeye, Jean Baptiste, Pierre Buyoya na Ndibantunganya Syvestre ma rais wa zamani tayari ni wanaseneti.
LEONARD NYANGOMA TAYARI AMEITOROKA NCHI KWA KUHOFIA USALAMA WAKE

BUJUMBURA:Mkuu wa chama cha CNDD Léonard Nyangoma akiwa pia msemaji wa muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC IKIBIRI, vyama amvavyo vilivyo pinga matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza la madiwani wa Mai 23, inasemeka kwamba tayari ameitoroka nchi sasa ni zaidi ya wiki. hii ni kutokana na hofu wa kutiwa nguvuni aidha kumaliziwa maisha zasema duru tofauti. Nyangoma ameitoroka nchi na kujificha kwa kuhofia maisha yake, amethibitisha hayo Alexis Sinduhije mkuu wa chama MSD kinacho jumuika katika muungano ADC IKIBIRI ambae aliliambia shirika la habari la ufaransa la AFP kwamba kiongozi huyo alionekana mara ya mwisho jijini Bujumbura Julay 20. Kiongozi huyo wa upinzani anashutumiwa na utawala baada ya kutowa tamko ambamo aliushutumu utawala kuhusika na mauaji huko Ruziba kwenye umbali wa kilometa 8 kusini mwa mji mkuu Bujumbura ambako ndege ya kijeshi na manuari vilitumiwa ilikuwasaka watu waliokuwa wamehusika katika mauaji ya wanamemba wa chama tawala CNDD FDD. waziri wa ulinzi aliomba afunguliwe mashtaka na polisi ilikuwa tayari kumtia nguvuni licha ya kinga ya muda alionayo kama mbunge.
mercredi 21 juillet 2010
WAZIRI WA ULINZI NCHINI BURUNDI AOMBA KESI UFUNGULIWE DHIDI YA MWANASIASA WA MRENGO WA UPINZANI LEONARD NYANGOMA
waziri wa ulinzi nchini Burundi meja jenerali Germain Niyoyankana ameitaka mahakama nchini humo kumfungulia kesi kiongozi wa upinzani wa chama CNDD bwana léonard Nyangoma kwa kile alicho kisema kiongozi huyo amekuwa akikashifu jeshi la Burundi. Hii ni baada ya kiongozi huyo wa mrengo wa upinzani kutowa matamshi kuhusu matukio ya ndege ya kijeshi iliovurumisha ma bomu na kuwamalizia maisha watu kadhaa. waziri wa ulinzi wa Burundi amesema mwanasiasa huyo alikuwa na malengo ya kuamsha hisia mbaya za wananchi hivo wakaidi serikali pindi alipo sema kwamba serikali ya Burundi yajihusisha na mauaji dhidi ya raia. Jeshi la burundi liliendesha siku za nyuma operesheni ya kuwasaka vijana waliosadikiwa kuhusika katika vitendo tofauti vya mauaji jijini Bujumbura vikiwemo vile vya ulipuaji ma bomu. Ndege za kijeshi na manuari ya kivita ilitumiwa ili kuwazuia vijana hao ambao inasadikiwa kuwa walikuwa na dhamira ya kutimkia nchini DRC wakipitia ndani ya ziwa Tanganyika. Hadi sasa haijulikani ni watu wangapi walioyapoteza maisha katika operesheni hiyo.dimanche 18 juillet 2010
JEAN CLAUDE KAVUMBAGU MHARIRI WA GAZETI NET PRESS AKAMATWA NA KUTIWA NGUVUNI
Mhariri wa gazeti la Net Press Jean Claude KAVUMBAGU alikamatwa jana jumamosi july 17 na polisi ya taifa kwa tuhuma ya kwamba alichapisha katika gazeti lake taarifa inayosema kwamba jeshi la Burundi na polisi vimezamilia hasa katika uporaji na mauwaji dhidi ya wananchi kuliko kulinda nchi yao. Mwanahabari huyo alikamatwa akiwa ofisini mwake. Wakili wake mtetezi Gabriel SINARINZI akihojiwa kuhusu kukamatwa kwa mteja wake na muungano wa redio za nchini Burundi amefahamisha kwamba Jean Claude KAVUMBAGU amekamatwa kinyume cha sheria kwani alipelekwa moja kwa moja katika jela kuu la Mpimba wakati kesi yake ilikuwa bado haijakatwa. Itafahamika kwamba Jean Claude KAVUMBAGU alihojiwa kwa muda wa masaa mawili kabla ya kupelekwa mbaroni.
jeudi 25 mars 2010
SILAHA ZILIZOMO MIKONONI MWA RAIA ZAENDELEA KUMALIZA MAISHA YA WANANCHI
Watu 3 wameuawa Mkoani Kirundo katika kijiji cha Renga zone ya Mukerwa tarafa ya Busoni katika usiku wa kuamkia alhamisi hii saa tatu na robo pindi majambazi waliokuwa na silaha walipo vamia familia moja. Miongoni mwa hayati hao ni baba na mkewe pamoja na mama yake. Katika tukio hilo dada wa hayati huyo alijeruhiwa.
Usalama mdogo umeripotiwa pia katika kijiji cha Migera Mkoani Nyabihanga. Watu wzenye silaha waliivamia nyumba ya mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Ntabahungu Gaspard. Baada ya kuwajeruhi watu 2 na risase wahalifu hao ndipo walianza kuwapora watu simu za mkononi, redio na pesa ambazo haijulikani idadi yake. Katika usiku huohuo mwananchi Nkurunziza Evariste wa kijiji cha Bugera tarafani Ndava alipigwa risase na wahalifu magotini na baadae wakatimka.
Usalama mdogo umeripotiwa pia katika kijiji cha Migera Mkoani Nyabihanga. Watu wzenye silaha waliivamia nyumba ya mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Ntabahungu Gaspard. Baada ya kuwajeruhi watu 2 na risase wahalifu hao ndipo walianza kuwapora watu simu za mkononi, redio na pesa ambazo haijulikani idadi yake. Katika usiku huohuo mwananchi Nkurunziza Evariste wa kijiji cha Bugera tarafani Ndava alipigwa risase na wahalifu magotini na baadae wakatimka.
mardi 9 mars 2010
MGOMO WA WAALIMU WAINGIA KATIKA SIKU YAKE YA PILI
BUJUMBURA:Mgomo wa waalimu wa shule za serikali kuisusia kazi leo umeingia katika siku ya pili.Shule nyingi zinazo patikana katika manispaa ya jij la Bujumbura zimefunga milango yake. Baadhi ya shule hata hivo hapa Mjini Bujumbura kama shule la kinama la msingi la kinama ya pili ni waalimu wachache pekee wanaofanya kazi. Hali kadhalika mgomo wa waalimu unatikisa shule za mikoani.Lakini tunaarifiwa kwamba Shule la kipili la mtakatifu Therese mkoani Gitega wanaofanya kazi ni waalimu wa kigeni.
Wakati huo huo Muungano mpya wa vyama vya waalimu katika shule za msingi SEEPBU unasema licha ya kwamba hawakujiunga na mgomo hata hivo wanaungana na madai ya waalimu ya masalia ya fedha katika upangiliaji upya wa vyeo vya waalimu.
Hata hivo mkuu wa chama hicho cha waaalimu SEEPBU Victor Nbabaniwe anasema wanatofautiana na wenzao kuhusu utaratibu wa kudai haki.Anasema inafaa kutumia majadiliano na serikali badala ya kuweka mgomo mbele. Hata hivo ameiomba serikali kuweka kwenye vitendo ahadi za waaalimu.
Wakati huo huo Muungano mpya wa vyama vya waalimu katika shule za msingi SEEPBU unasema licha ya kwamba hawakujiunga na mgomo hata hivo wanaungana na madai ya waalimu ya masalia ya fedha katika upangiliaji upya wa vyeo vya waalimu.
Hata hivo mkuu wa chama hicho cha waaalimu SEEPBU Victor Nbabaniwe anasema wanatofautiana na wenzao kuhusu utaratibu wa kudai haki.Anasema inafaa kutumia majadiliano na serikali badala ya kuweka mgomo mbele. Hata hivo ameiomba serikali kuweka kwenye vitendo ahadi za waaalimu.
VIONGOZI WA MKOA WA KAYANZA WAMEPIGA MARUFUKU WAGENI KUINGIA NA WANAFUNZI KUTOKA KATIKA SHULE LA KIPILI LA KAYANZA
BUJUMBURA:Wakuu wa mkoa wa Kayanza wamechukua hatua kali za kiusalama katika shule la kipili la Kayanza baada ya kuripotiwa hali ya mtafaruku baina ya wanafunzi ,kukiwa ba chuki za chini kwa chini za kikabila na kisiasa.
Hatua hizo ni pamoja na kupiga marufuku nenda-rudi za wanafunzi,kupokea wageni shuleni hapo aidha kuondoka nje ya shule.Pia matumizi ya simu za mkononi yamepigwa marufuku.
Kwa mujibu wa muandishi wa habari wa radio Burundi mkoani hapo, Gavana na mkuu wa tarafa ya Mkoa wa Kayanza pamoja na wakuu wa usalama walikuwa jumatatu hii shuleni hapo kutuliza nyoyo wanafunzi na kuwaasa kujiepusha na hisia zote za mtengano zinazoweza kutishia usalama wa shule na wanafunzi
Mkoani Gitega nako tunaarifiwa kwamba wakuu wa shule la kipili la Notre Dame de la Sagesse maarufu CND wamechukua hatua ya kuwafuta wanafunzi sita wakituhumiwa kwamba wamekuwa wanawashawishi wanafunzi shuleni hapo wasitumie chakula cha maharagwe ambayo yanadaiwa kwamba sio mazuri.
Hatua hizo ni pamoja na kupiga marufuku nenda-rudi za wanafunzi,kupokea wageni shuleni hapo aidha kuondoka nje ya shule.Pia matumizi ya simu za mkononi yamepigwa marufuku.
Kwa mujibu wa muandishi wa habari wa radio Burundi mkoani hapo, Gavana na mkuu wa tarafa ya Mkoa wa Kayanza pamoja na wakuu wa usalama walikuwa jumatatu hii shuleni hapo kutuliza nyoyo wanafunzi na kuwaasa kujiepusha na hisia zote za mtengano zinazoweza kutishia usalama wa shule na wanafunzi
Mkoani Gitega nako tunaarifiwa kwamba wakuu wa shule la kipili la Notre Dame de la Sagesse maarufu CND wamechukua hatua ya kuwafuta wanafunzi sita wakituhumiwa kwamba wamekuwa wanawashawishi wanafunzi shuleni hapo wasitumie chakula cha maharagwe ambayo yanadaiwa kwamba sio mazuri.
vendredi 9 octobre 2009
HALI YA PURUKUSHANI BAINA YA POLISI NA WAKIMBIZI HUKO GIHINGA
kumetokea hali ya mvutano kati ya Polisi wa uslama wa raia nchini Burundi na wakimbizi wa congo wa kabila la Banyamulenge. Tukio hilo limetokeya ktk kambi ya Gihinga iliyo mkoani Mwaro kati kati mwa Bdi umbali wa kilometa 70 hivi na mji mkuu Bujumbura, ambako askari polisi wamewafiatuliya risase wakimbizi banyamulenge na wawili miongoni mwao kujeruhiwa, huku wengine watatu wakizirayi kutokana na miliyo ya risase kambini hapo Gihinga. Kambi hiyo ya Gihinga ilikuwa imewapa hifadhi wakimbizi Banyamulenge 2317 kutoka nchi jirani ya RDC. Septemba 21 ndipo Shirika la UM linalo wahudumiya wakimbizi UNHCR liliamuru kusitisha huduma zake zote kwa wakimbizi hao, baada ya wakimbizi hao kupinga kuhamishiwa ktk kambi ya bwagiriza iliyo ktk mkoa wa Ruyigi mashariki mwa Bdi kwenye mpaka na Tanzania. Septemba 30 shirika la UNHCR lilitangaza kuwa kambi ya Gihinga imefungwa licha ya wakimbizi hao kusaliya kambini huku miongoni mwao 264 wakikubali kuhamishiwa bwagiriza mkoani Ruyigi. Hatua hiyo ilipelekeya wakimbizi hao kuchukuwa uwamuzi wa kurudi kwa mguu nchini kwao RDC, hatua ambayo imeanza kutekelezwa jumanne hii.
samedi 12 septembre 2009
WANASIASA NCHINI BURUNDI WATOFAUTIANA KUHUSU SHERIA YA UCHAGUZI
BUJUMBURA: Kumekuwa na hisia tofauti baina ya wanasiasa nchini Burundi kuhusiana na sheria ya uchaguzi iliopasishwa bungeni usiku wa alhamis kuamkia ijumaa septemba 11, 2009. Chama Sahwanya FRODEBU kimesema kufurahishwa na hatuwa hiyo ya kupasisha sheria ya uchaguzi bungeni, lakini hata hivo mwenyekiti wa chama SAHWANYA FRODEBU Leonce Ngendakumana amesema kuwa na wasiwasi hasa kwamba kadi moja ya uchaguzi iliokuwa ikitetewa na chama hicho haikupasishwa kaika muswada huo. upande wake msemaji wa chama FNL Bosco HAVYARIMANA amesema kuwa wabunge wamekwenda kinyume kabisa na maafikiano waliokuwa wamekubaliana siku za nyuma. kiongozi huyo amesema kuwa kiwango cha dhamana kinacho takiwa kwa wagombe viti mbalimbali vya uchaguzi hakina sababu za kuwepo. upande wake mwenyekiti wa chama CNDDLéonard Nyangoma amesema ni aibukubwa sana kwa taifa la Burundi. upane wake amesema sheria hiyo ya uchaguzi inakuja kurejesha nyuma hatuwa za demokrasia nchini Burundi ukilinganisha na sheria.
BAADA YA MVUTANO WA SIKU NZIMA, HATIMAE WABUNGE WAMEPASISHA SHERIA ZA UCHAGUZI SAA TISA USIKU
BUJUMBURA le 11.9.2009:Hatimae wabunge nchuini Burundi wamepasisha muswada wa sheria uhusuo uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Tangu saa tatu asubuhi alhamis Septemba 2009, wabunge walitakiwa kujadili na kupasisha muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi nchini Burundi. Kutokana na utata uliokuwemo katika sheria hizo, ilikuwa vigumu kupatikana muafaka, hadi saa tisa usiku wa kuamlia ijumaa septemba 11, wabunge walifikia muafaka na kusaini sheria zihusuzo uchaguzi wa 2010. miongoni mwa walioafikiana ni pamoja na mpangilio wa uchaguzi utaoanzia kwa viongozi wa madiwani na baadae kufuatia uchaguzi wa rais, utaofuatiwa na na wa bunge na seneti na kuhitimishwa kwa ule wa viongozi wa ngazi za china. Ama kuhusu kadi ya uchaguzi, wanasiasa hao wameafiki kutumia kadi tofauti na vijisanduku 2. kimoja kitapokea kadi iliopiga kura na nyingine itayo tupwa katika kijisanduku maalum kitachokuwa kimeandaliwa. Ili kuepusha wizi na udanganyifu, kadi zote zitahesabiwa, zile zilizo chaguliwa na zile zilizo tupwa sehemu kutakokutikana na udanganyifu sehemu hiyi uchaguzi utafutwa na baadae kuandaliwe mwingine katika kipindi kisichozidi siku 5. kuhusiana na dhamana anayo takiwa kutowa mgombea kiti cha urais imesalia kuwa franka za Burundi millioni 15, pesa hizo zitarejeshwa iwapo mgombea hatofikisha asilimia 5 ya kura zitazopigwa nchi nzima. Mgombea kiti cha ubunge atalipa dhamana inyo lingana na franka za Burundi laki 5 huku , mgombea kiti cha uanaseneta akilipa franka za Burundi laki 4. Pesa hizo zitarejeshwa iwapo wagombea hao hawatofikisha asilimia 2 ya kura zitazopigwa kote nchini. Wabunge walikubaliana pia kuhusu kufutwa ubunge kwa mbunge ataekuwa amekitoroka chama chake na kujiunga na chama kingine swala ambalo lililo zusha utata, hatimae wabunge wamekubalina na swala hilo.
Inscription à :
Articles (Atom)